MANCHESTER United wanatarajia
kuipa Arsenal kipigo cha pili msimu huu wanapokutana leo katika mechi ya
ligi kuu England uwanja wa Old Trafford.
Louis van Gaal alishinda 2-1dhidi
ya Arsenal katika uwanja wa Emirates mwezi novemba mwaka jana na
leo anahitaji kushinda kwa mara ya pili msimu huu.
leo anahitaji kushinda kwa mara ya pili msimu huu.
Baada ya kupoteza mechi tatu
mfululizo, United walishinda dhidi ya Crystal Palace wiki iliyopita na
kimahesabu wanahitaji pointi moja tu kufuzu ligi ya mabingwa Ulaya msimu
ujao, ingawa Liverpool wanaoshika nafasi ya tano wapo nyuma kwa pointi
sita, wana wastani mbaya wa magoli ya kufunga na kufungwa.
Gunners ambao walishinda 2-1
dhidi ya Man United Old Trafford katika mechi ya raundi ya sita ya kombe
la FA, leo wanahitaji kushinda ili kuipiku Man City kushika nafasi ya
pili msimu huu.
HABARI ZA TIMU
Wayne Rooney na Luke Shaw
wanaikosa mechi ya leo kutokana na majeruhi waliyopata wiki iliyopita
kwenye mechi dhidi ya Crystal Palace.
Marcos Rojo, Angel Di Maria na
Robin van Persie wako hatarini kuikosa mechi hii wakati Michael Carrick
na Rafael wako nje kwa mechi zote za ligi kuu zilizosalia.
Danny Welbeck anakosa nafasi ya
kucheza dhidi ya timu yake ya zamani kwasababu ya majeruhi ya goti na
Mathieu Debuchy hayupo pia.
TAKWIMU MUHIMU
Manchester United hawajawahi
kufungwa katika mechi 7 za nyumbani dhidi ya Arsenal (Wameshinda 6, sare
1) tangu walipofungwa 1-0 mwezi septemba 2006.
Wayne Rooney amefunga magoli 11
dhidi ya Arsenal katika mechi za ligi kuu England, lakini amefunga
magoli mengi zaidi dhidi ya Aston Villa (13) na Newcastel (12).
United hawajaruhusu kufungwa
zaidi ya goli moja katika uwanja wa nyumbani dhidi ya Arsenal na
kupoteza mechi ya ligi tangu februari 1979.
Arsenal inaweza kuwa timu ya nne
kihistoria kuifunga Man United mara mbili Old Trafford katika msimu huo
huo. Timu nyingine zilizowahi kufanya hivi ni Chelsea (2004/2005),
Tottenham (1989/90) na Aston Villa (1919/20).
Manchester United wameshindwa
kuzuia kufungwa goli katika mechi saba walizocheza na mara ya mwisho
kucheza mechi 8 bila kuruhusu nyavu zao kuguswa ilikuwa septemba 2001.
Arsenal wameshinda mechi tano
zilizopita za ugenini, huu ni mwenendo mzuri zaidi kuwahi kutokea tangu
walipofanya hivyo septemba 2013 (walishinda mechi 8).
No comments:
Post a Comment