Raia wa Uingereza jana walikuwa na kazi
moja ya kumchagua kiongozi mpya atakayewaongoza kwa muhula mwingine
baada ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu.
Chama cha Conservatives kilikua na upinzani mkali dhidi ya
Labour lakini kura ya Raia hao imeangukia kwa Waziri mkuu wa nchi hiyo David Cameron kushinda kiti cha kuongoza Taifa hilo kubwa duniani kupitia chama chake cha Conservatives.
David Cameron amechaguliwa kwa awamu ya pili na ushindi huo umekuja baada ya kushinda viti 323 alivyohitajika kushinda.
Baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo kiongozi wa chama cha Labour cha Uingereza, Ed Miliband
amewaambia wanaharakati wa chama hicho kwamba anajiuzulu kama kiongozi
wa chama hicho kufuatia matokeo yasiyo ya haki ya uchaguzi huo.
David Cameron anarejea madarakani bila
idadi kubwa ya wabunge kwa kuwa Chama cha Conservative kitalazimika
kuunda serikali ya muungano.
Miliband amempongeza Waziri mkuu David
Cameron kwa kuchaguliwa kwa awamu ya pili na amesema kuwa anachukua
jukumu la kushindwa kwa chama chake katika uchaguzi huo.
No comments:
Post a Comment