MTIFUANO wa Ligi
ya Mabingwa Ulaya unaendelea kuwa mtamu baina ya miamba ya soka barani humo Barcelona na
Bayern München kushuka dimbani Camp Nou kwa ajili ya kutafuta tiketi ya kutinga
fainali ya michuano hiyo.
Wakati
hayo yakijiri vitabu vya kumbukumbu za kihistoria vya Shirikisho la Soka la
Ulaya (UEFA) vinaonyesha Hispania imeendeleza rekodi yake ya kuwa na timu
katika nusu fainali kwa misimu 16 ukianza msimu wa 1992/93.
Hispania
imeshikilia rekodi hiyo ikikosa timu misimu 6 tu katika misimu 22 huku wawakilishi 26 kati ya 88 waliotinga
hatua hiyo wametoka nchini humo.
England
imeshika nafasi ya pili kwa kuwa na wawakilishi 20 kati ya 88 sawa na asilimia
22.7 ikilinganishwa na 29.5 ya Hispania.
Msimu
huu ni wa tisa kwa nchi ya England kukosa timu kwenye hatua ya nusu fainali.
Italia
na Ujerumani (timu 14), Ufaransa (timu 6), Uholanzi (4), Ureno (2), Ugiriki na
Ukraine (1).
Uimara
Gerrard
Pique amekaririwa akisema hajawahi kuona safu ya ushambuliaji kama MSN–Messi,
Suarez na Neymar tangu aanze kuitumikia Barcelona.
Bayern
chini ya kocha aliyeifanikisha Barcelona Pep Guardiola inatarajiwa
kumiliki mpira zaidi lakini uimara wa
Bavarians upo zaidi ya hapo kwani wanaweza kucheza zaidi ya mifumo iliyonayo
Barcelona.
Uwepo
Roberto Lewandowski katika ushambuliaji ni faraja kubwa akiungwa mkono na
Thomas Müller, Mario Gotze Frank Ribery na Jerome Boateng utaisumbua sana ngome
ya Blaugrana.
Udhaifu
Barcelona
ina uwezo wa kushika mchezo kama timu huku ikikosa uwezo wa mmoja mmoja (man-for-man)
ambao Bayern wanao hivyo kama wote watataka kukaa na mpira basi uwezo wa Barca
kusimama kwa mchezaji mmoja moja hautakuwepo.
Kwa
upande wao Bayern watamkosa Arjen Roben ambaye ni majeruhi huku kukiwa na
hatihati ya kumkosa Frank Ribery.
Tukirejea
katika mechi mbili za Bayern katika Bundesliga iliruhusu mashambulizi ya ghafla
kutoka kwa Wolfsburg na Möenchengladbach kama wasiporekebisha itawagharimu.
No comments:
Post a Comment