Ghana, Algeria na Gabon zote ziliangusha karata ya bahati nasibu
kwenye Shirikisho la Soka Afrika CAF ambapo kila moja ilijipa nafasi ya
kushinda ili kuteuliwa kuandaa Michuano ya CAF mwaka 2017, tayari leo
Dunia imejua nani kaibuka na ushindi kati yao.
Taarifa iliyotolea leo April 8 2015 kutoka Cairo, Misri ni kwamba Shirikisho hilo la soka Afrika CAF limetangaza kuwa Gabon imechaguliwa kuandaa michuano ya Kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2017.
Libya ndio nchi iliyokuwa iandae michuano hiyo lakini iliomba iondolewe kwenye nafasi hiyo kutokana na hali ya usalama kuwa sio nzuri.
Shirikisho la soka Afrika CAF limeichagua Gabon ambayo ilikuwa ikigombea nafasi hiyo pamoja na Ghana pamoja na Algeria ambayo huenda imepoteza nafasi hiyo kutokana na hali ya usalama katika viwanja vyake baada ya tukio la kifo cha mchezaji wa Cameroon, Albert Ebosse mwaka 2014.
No comments:
Post a Comment