08 April, 2015

Rekodi nyingine kwa Ronaldo.


Cristiano Ronaldo


Mchezaji bora wa dunia na nyota wa Real Madrid Cristiano Ronaldo usiku huu ana nafasi ya kuweka rekodi nyingine katika msururu wa rekodi nyingi ambazo ameziweka akiwa anaichezea klabu hii ya Hispania .
Ronaldo ambaye siku tatu zilizopita aliwahukumu Granada kwa kuwafunga mabao 5 katika ushindi wa  9-1 atafikisha idadi ya mabao 300 katika michezo ya ushindani endapo atafunga bao moja kwenye mchezo ambao Real Madrid inacheza dhidi ya Rayo Vallecano .
Ronaldo hadi sasa amefunga jumla ya mabao 47 katika michezo 41 ya michuano mbalimbali na anamzidi mpinzani wake Lionel Messi kwa mabao matatu kwenye ligi ya Hispania .
Historia inaonyesha kuwa Ronaldo amefunga mabao manne kwenye tisa dhidi ya Rayo Vallecano hali inayoonyesha kuwa hatakuwa na wakati mgumu kuzifumania nyavu na kutimiza mabao 300 .

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...