Hadi dakika ya 33 ya mchezo huo,
mwamuzi wa mtanange huo anapuliza kipyenga kiashilio kuwa mchezo
hautaendelea, Wenyeji Stand United walikuwa wakiongoza kwa bao 1-0,
ambapo Goli hilo lilifungwa na Haruna Chanongo kunako dakika ya 12.
Mbali na mchezo huo wa leo
kuvunjika, Pia jana Mtanange kati ya Simba na Kagera Sugar ulishindwa
kuchezeka baada ya Uwanja huo kujaa maji katika maeneo muhimu ya Uwanja
kama Laangoni na sehemu nyingine.
Kufatia uamuzi huo sasa timu hizo zitakutana kesho jumatatu endapo hari ya hewa itaruhusu.
No comments:
Post a Comment