Kutoka kwenye michango ya kwenye vibubu kutoka kwa mashabiki hadi kufanikiwa kuingia kwenye ligi kuu na rekodi kubwa kabisa. Club ya Bournemouth imefanikiwa kuingia kwenye ligi inayoangaliwa sana kuliko ligi zote duniani EPL kwa mara ya kwanza tangu ianzishwe.
Baada ya kufunga Bolton 3-0 wamejihakikishia nafasi ya kucheza kwenye ligi kuu msimu ujao labda wakifungwa magoli 19-0 na Charlton kwenye mechi inayofuatia.
Kocha wa Bournemouth anatajwa kama the special one kutoka England au akifananishwa labda na Pep Guardiola kwasababu ameiongoza club kuwa promoted mara tatu ndani ya miaka 6 tu. Ukiangalia umri wake ni miaka 37 tu, unaweza kuona kwamba ana nafasi ya kufanya mambo mengi mbele ya maisha yake ya soka.
Bournemouth inakua ni club ya 47 kucheza ligi kuu kama mambo yakienda kama vile wao wanavyofikilia kwamba Charlton hawatawafunga magoli 19-0. Kuharibu furaha yao club ya Charlton ime-tweet kwamba “Bournemouth celebrating like they’ve completely ruled out a 19-0 defeat at The Valley on Saturday. We’ll see”. So, wanawapa onyo kwamba wasishangilie kwasababu mechi bado haifanyika na lolote linaweza kutoka.Hii ni mechi tamu sana ya kuiangalia kama wewe ni mpenda soka. Bournemouth FC kwa jina la utani wanaitwa The CherriesCallum Wilson amefunga magoli 20 kwenye ligi msimu huu kwa kwenye timu ya Bournemouth
No comments:
Post a Comment