Mwanamitindo wa TZ ambaye yuko kwenye
HEADLINES za Kimataifa.. Nimekutana na kitu kinachohusu yeye mtandaoni,
nikaona kwa sababu ni mtu wetu basi niisogeze hii ili watu wake pia
waone.
Kaingia kwenye HEADLINES za Magazine kubwa duniani, BLACK ENTERPRISE ambao
wamefanya nae exclusive interview, mengi kayasema hapa
mengine hata sikuwahi kuyajua kutoka kwake.. kumbe ishu ya kuingia kushiriki Miss Universe hata hakuwa na idea ya kitu anachokifanya, aliingia kwa kujifurahisha tu !!
mengine hata sikuwahi kuyajua kutoka kwake.. kumbe ishu ya kuingia kushiriki Miss Universe hata hakuwa na idea ya kitu anachokifanya, aliingia kwa kujifurahisha tu !!
Kingine alichokiongea ni ishu ya Flaviana Matata Foundation, taasisi ambayo aliianzisha kwa ajili ya kusaidia wasichana yatima kwenye masuala mbalimbali ikiwemo mahitaji muhimu ya Shule.Niliwahi
kumuona marehemu mama yangu akisaidia watoto wengine kuwapeleka shule..
Nilikuwa mdogo sana lakini alikuwa akituambia na ndugu zangu umuhimu wa
kusaidia watu ambao wanahitaji msaada.. Nilianzisha FMF kwa ajili ya
moyo wa kujitolea..“– Flaviana Matata.
“Jitihada nnazozifanya kusaidia wasichana kupata elimu itakuwa ni kitu ambacho kila mtu anaweza kukipongeza..“– Flaviana Matata.
Safari ya staa wetu wa mitindo
inaendelea yani, kwenye exclusive hiyo amesema moja ya changamoto
iliyopo TZ ni watu wachache kutoa support kwenye misaada anayotooa kwa
kuwa ni wachache ambao wanajua maana ya kujitolea kwa jamii.
Tumeona zaidi ya mara mbili staa huyu
anatoa misaada mashuleni, anahitaji support yako pia mtu wa nguvu ili
kuifanikisha, unaweza kumfollow kwenye Twitter na Facebook @FlavianaMatata, Instagram unaweza kumcheki kwa kubonyeza hapa pia @flavianamatata
Mawerenewz.blogpot.com ndio mtandao wako wakipekee
unaokupa habari za BURUDANI,MICHEZO,SIASA, na HABARI MBALIMBALI ZA KIMATAIFA
pamoja na KITAIFA
Endelea kutembelea MTOKA MBALI pia nifuate twitter>>>@mawere3,
facebook>>>Francis mawere the jr, Instagram>>>Zawadi_mawere.
AKSANTE.
No comments:
Post a Comment