MWANAMUZIKI maarufu wa Nigeria anayejiita ‘Eja Nla’ (Samaki Mkubwa) ambaye jina lake halisi ni , Dapo Oyebanjo, akijulikana pia kama D’Banj, hakufika mahakamani wakati wa kuanza kwa kesi ambayo anashitakiwa kwa kutolipa deni
Kesi hiyo ilikuwa ianze kuunguruma Machi 30 mwaka huu kwenye mahakama ya Multi-Door Courthouse, eneo la Obalende, Lagos,lakini mwanamuziki huyo hakufika. Mlalamikaji , Henry Ojogho, naye hakufika.
Hata hivyo, wakili wake (D’Banj) aitwaye Dele Adeshina, alifika mahakamani.
Wakati huohuo, hakimu aliyepangwa kusikiliza kesi hiyo, Bi Oyebanji, aliiahirisha hadi Mei 7 mwaka huu itakaposikilizwa tena.Ojogho, ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa kampuni la Broron Group and MindHub Technologies, alidai kwamba D’Banj ambaye ndiye mmiliki wa kampuni la DB Records, alimkopa Naira milioni 60 lakini akakataa kuzilipa kama alivyoahidi.
No comments:
Post a Comment