14 April, 2015

Baada ya Diamond kumkataza kwenda A Kusini kujifungulia, Hii ndiyo hospitali Zari anayo endea kliniki hapa Bongo


 Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amemzuia mama kijacho wake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kwenda kujifungulia nje ya Bongo pindi mambo yatakapokuwa tayari.
Habari zilizonyakwa na Ijumaa Wikienda kutoka kwenye chanzo cha ndani ya familia ya Diamond zilieleza kwamba, tayari jamaa huyo amemuanzishia
Zari kliniki Bongo.“Yaani Diamond hataki kabisa Zari kwenda kujifungulia South Africa (Sauzi). Anataka kila kitu kifanyike hapahapa Bongo. Tayari amemuanzishia kliniki kwenye Hospitali ya AMI (ipo Masaki, Dar),” kilitonya chanzo hicho.
Akizungumzia ishu hiyo, Diamond alisema kuwa anatamani kuwa karibu na mama kijacho wake huyo hivyo ni kweli anataka mwanadada huyo ajifungulie Bongo.

Diamond au Baba Kijacho alisema lengo la kufanya hivyo ni ili iwe shangwe kwa familia nzima tofauti na atakapojifungulia nje ambapo familia italazimika kusafiri kwenda kumuona Chibu Junior.
Kwa mujibu wa Diamond, Zari ambaye ni mama wa watoto watatu akifukuzia huyo wa nne anatarajia kujifungua kati ya mwezi Julai au Agosti, mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...