09 September, 2016

Video: Pipi ft Nikki wa Pili – Hafai

Msanii Pipi mwenye sauti tamu katika mziki wa Bongo fleva ameachia video yake mpya ya wimbo “Hafai”, amemshirikisha mkali wa Hiphop Nikki wa Pili. Video imeongozwa na kampuni ya Blue Image. Unaweza Kuupakua wimbo huo(Audio) kwa kubonyeza DOWNLOAD hapo chini

AudioMPYA:Bushoke- Mpita Njia

Ni Headlines za msanii kutoka Bongoflevani, Bushoke ambae ametuletea hii single yake mpya iitwayo ‘Mpita Njia’, wimbo umetayarishwa na producer Ema The Boy na Alan Mapingo. Bofya Download hapo chini kuupakua waimbo huo.

Video: Malaika "Rarua"

Hii ni time nyingine tena ya kuenjoy na mdundo mpya kutoka kwa staa wa bongo flavour Malaika ambaye alishawahi kumiliki mdundo wa ‘salesale‘ aliomshirikisha producer Mensen Selekta na sasa kaileta hii ya ‘Rarua

Video: TID ft Joh Makini – Confidance

Video mpya kutoka kwa msanii TID ya wimbo “Confidance”, amemshirikisha Joh Makini. Video imeongozwa na kampuni ya Kwetu Studios. Downlaod Audio hapo chini

Serena Williams atupwa nje kwenye michuano ya US Open

Serena Williams ameendelea kuharibu kwenye mashindano ya tennis baada ya hapo jana kuondolewa kwenye nusu fainali ya michuano ya US Open na mchezaji wa Jamhuri ya Czech, Karolina Pliskova.
381880bc00000578-0-image-a-4_1473382194216
Kwenye mchezo huo Karolina alifanikiwa kushinda kwa seti 6-2, 7-6 (3) katika mchezo uliofanyika kwa muda wa saa moja na dakika 26. Kwa sasa Pliskova atakutana na Kerber kwenye mchezo wa fainali siku ya Jumatatu.
38188a3e00000578-3780869-image-a-22_1473382710662
Mapema mwezi Agosti mwaka huu Serena na ndugu yake Venus Williams walitolewa kwenye raundi ya kwanza ya mchezo wa tennis wa wanawake wawili wawili kwenye michuano ya Olimpiki.
38187ad500000578-3780869-image-a-19_1473382609664
Serena alikuwa anatarajia kufikisha mataji 23 ya grand slam kwenye michuano hiyo na kuvunja rekodi ya Steffi Graf ya mataji 22 ambayo wanafanana kwa sasa.

06 September, 2016

New AUDIO: Chibau Mtoto Wa Pwani Ft.Nay TrueBoy - KAWIMBO

Chabai mtoto wa Pwani ni moja wa wasanii wa bongo flava ambao wamekaa kimya kwa muda mrefu, ila safari hii kaja na ngoma ijulikanayo kwa jina la KAWIMBO akiwa amemshirikisha rapper Nay TrueBoy, ngoma imetengenezwa na Producer Mr T-Touch. Bofya DOWNLOAD hapo chini kuupakua wimbo huo.

Wayne Rooney akerwa na mjadala juu yake

kaptein  
Nahodha wa timu ya Uingereza Wayne Rooney amesema kuwa majadiliano yanayoendelea kuhusu shughuli zake ndani ya timu hayana maana.

Rooney ambaye amecheza mechi yake ya 116, akicheza kama kiungo siku ya jumapili walishinda 1-0 dhidi ya slovakia, ambayo ilikuwa ni mechi ya kwanza chini ya meneja mpya Sam Allardyce's.Allardyce amesema kuwa mechi iliyopita hakuwa na la kusema kuhusu nafasi ya Rooney ilikuwa ipi na kucheza alivyotaka.
Rooney mwenye miaka 30 alisema " Nilicheza kwa nafasi yangu ili kusaidia timu yangu kushinda mchezo, japo mengi yalifanyika juu yake"
Akiongea na Sky Sport, kapteni wa timu ya Manchester United aliongeza kuwa" Nimekuwa nikifanya kazi yangu yote na ghafla ikawa habari kubwa, si jambo kubwa na nadhani kuna kutoeleweka kwa kiasi kikubwa juu ya hilo"
Nafasi ya Rooney kwenye Klabu yake na nchi imekuwa ikijadiliwa kwa kiasi kikubwa msimu huu na kwa rekodi ya wafungaji nchini Uingereza.

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...