Kwenye mchezo huo Karolina alifanikiwa kushinda kwa seti 6-2, 7-6 (3) katika mchezo uliofanyika kwa muda wa saa moja na dakika 26. Kwa sasa Pliskova atakutana na Kerber kwenye mchezo wa fainali siku ya Jumatatu.
Mapema mwezi Agosti mwaka huu Serena na ndugu yake Venus Williams walitolewa kwenye raundi ya kwanza ya mchezo wa tennis wa wanawake wawili wawili kwenye michuano ya Olimpiki.
Serena alikuwa anatarajia kufikisha mataji 23 ya grand slam kwenye michuano hiyo na kuvunja rekodi ya Steffi Graf ya mataji 22 ambayo wanafanana kwa sasa.
No comments:
Post a Comment