Wenger: Wachezaji wa Afrika wamenifaa sana katika soka

Arsene Wenger ameongoza Arsenal kwa miaka 20
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger ameiambia BBC kuwa wachezaji kutoka nchi za Afrika wamekuwa wenye umuhimu mkubwa katika taaluma yake ya miaka 20.

Wenga alikuwa akizungumza wakati wa mkutano wake wa kawaida na waandishi wa habari kabla ya mechi ambapo pia alitunukiwa kwa kukiongoza klabu hicho kwa miongo mwili.Nwankwo Kanu wa Nigeria alikuwa mmoja wa wachezaji waliokuwa wenye umuhimu mkubwa kwa Arsene
Akiwa mwenye uso uliotabasamu, Wenger amesena kuwa wachezaji kutoa Afrika wana moyo, wenye ubunifu na nguvu, masuala ambayo ni vigumu kuyapa kwenye mchezo.

Aliwataja wachezaji akiwemo Nwanko Kanu wa Nigeria, Kolo Toure wa Ivory Coast na gwiji raia wa Liberia George Weah, ambaye alikuwa meneja wake katika klabu ya Monaco nchini Ufaransa, kama wachezaji watatu waliokuwa na uswawishi mkubwa katika taaluma yake.

Comments

Popular posts from this blog

Viashiria 6 ni kwa nini unatakiwa kubadili Maisha yako Leo

Furaha ya kweli inaletwa na wewe mwenyewe.