Kampuni ya Snapchat imezindua miwani ya aina yake yanayomuezesha mtu kupiga video na kuisambaza katika mtandao huo wa kijamii.
Snapchat imejiongezea sifa kwenye mitandao ya kijamii inayotumiwa kutuma ujumbe, zikiwemo picha na video ambazo hufutwa baada ya kuonekana mara moja.
Lakini kifaa hicho kipya na kampuni hiyo kubadilisha jina kutoka Snapchat na kujiita Snap, zinadhihirisha azma ya kampuni hiyo kupita kiwango cha kuwa mtanadao wa ku chati.
Katika tangazo lake la biashara, Snap inasema miwano hiyo ya kutuma video ina lensi ya ukubwa wa digri 115, iliyo na upana zaidi kuliko kamera za kwenye simu za kisasa.
Na ina uwezo wa kurekodi video kwa hadi sekundi kumi kwa mara moja.
Picha hizo zinaweza kutumwa moja kwa moja kwenye mtandao huo wa kijamii ili mtu aweze kuzisambaza kwa wafuasi wengine wa mtandao huo.
Mkurugenzi mkuu wa Snap mwenye umri wa miaka 26, Evan Spiegel, ametaja miwani hiyo kama chombo kinachomuezesha mtu kuona kumbukumbuku nzuri kama walivyoiptia kwa mara ya kwanza.
No comments:
Post a Comment