04 September, 2016

Mkutano wa mataifa ya G-20 waanza Uchina

Viongozi wa mataifa yenye uwezo mkubwa duniani wakongamana nchini Uchina
Mkutano wa mataifa yenye uwezo mkubwa duniani, G-20 umeanza rasmi siku ya Jumapili mjini Hangzhou huko China, huku viongozi wa mataifa hayo wakianza kuhutubu.
Katika misururu ya mikutano ya leo itakuwa tu hotuba kutoka kwa viongozi wa mataifa wanachama.
Maswala yanayojadiliwa ni pamoja na swala muhimu la usalama katika maeneo ya bahari ya kusini mwa China.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, kucheleweshwa kwa swala la kifedha, katika harakati za kufufua uchumi hususan miongoni mwa mataifa madogo madogo yanayokuwa kiuchumi.
Aidha amesifu Marekani na Uchina kwa kuridhia muafaka wa Paris kuhusiana na mabadiliko ya hali ya hewa.
China imefanya kila iwezalo kuhakikisha kuwa mkutano huo unafaulu.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...