Mwanariadha Mjamaica Usain Bolt
ameshinda mbio za mita 200 katika michuano ya Olympics huko Rio nchini
Brazil na kujinyakulia medali ya dhahabu ya pili baada ya kunyakua ya
michuano ya mbio za mita 100.
Mapema wiki hii alidhihirisha kuwa ni mwamba wa mbio fupi pale aliposhinda mbio za mita 100 na kunyakuwa medali ya dhahabu.
Katika matokeo mengine Marekani imenyakulia medali nyingine nne za dhahabu ikiwemo ya mwanariadha wake Ashton Eaton.
No comments:
Post a Comment