05 August, 2016

Guardiola: Naisubiri kwa hamu mechi ya klabu bingwa

Mkufunzi mpya wa manchester City Pep Guardiola

Mkufunzi wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola amesema kuwa mechi ya timu hiyo ya kufuzu kwa kombe la klabu bingwa Ulaya ni mechi muhimu zaidi msimu huu.

Itakuwa aibu kubwa kwa klabu hiyo na meneja wake mpya iwapo itashindwa kufuzu.
Kati ya klabu tano ambazo City huenda wakakutana nazo ni klabu ya AS Roma pekee ambayo ilikutana nayo katika mechi za makundi mwaka 2014-15 ikipata sare katika uwanja wa Etihad na baadaye kupata ushindi wa mabao 2-0 katika uwanja wa Stadio Olimpiko kufuatia mabao ya Samir Nasri na Pablo Zabaleta na hivyobasi kufuzu katika robo fainali ya michuano hiyo.
City haijawahi kucheza dhidi ya Steaua Bucharest,Monaco ama Rostov ,lakini imecheza na timu kutoka Romania,Ufaransa,Urusi katika historia yao ya Ulaya.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...