27 July, 2016

Roger Federer ametangaza Kutoshiriki michuano ya Olympiki mwaka huu.


 
Tangazo lake hili linakuja kufuatia maumivu ya goti aliyoyapata na kufanyiwa upasuaji mwezi februari hali iliyomsababisha kuzikosa French Open zilizofanyika mwezi Mei.

Mapumziko haya ya Federer yatamfanya kuikosa michezo yote ya msimu wa mwaka huu. Amesema anahitaji kujijenga upya iwapo anataka kuendelea na mchezo wake wa Tenisi.
Kupitia ukurasa wake wa Facebook amesema anasikitika kwa kutoiwakilisha nchi yake ya Uswisi huko Brazil katika Olympiki na anajisikia vibaya kupoteza muda wa msimu uliosalia.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...