21 June, 2016

Waheshimu wazazi wako katika Uzee wao maana.....


feature image 62

Mzee mmoja mwenye miaka ipatayo 80 alikua ameketi katika sofa nyumbani kwake na mwanawe mwenye umri wa miaka 45, Ghafla akatokea njiwa katika dirisha huku njiwa yule akiwa anaipiga kelele. Yule Baba akamwambia mwanawe "Ni nini hicho?", mwanawe akamjibu "Ni njiwa", Baba akamuuliza tena kwa mara ya pili "Ni nini Hicho?" mwanae akamjibu "Baba nimekwambia ni njiwa".

Baada ya Muda kidogo, Baba yule alimuuliza mwanawe kwa mara ya Tatu "Ni nini hicho?" mwanawe yule akajawa na ghadhabu na kumjibu baba yake "Ni njiwa, ni njiwa". Baada ya Muda tena, baba yule alimuuliza mwanawe "Ni nini hicho?" safari hii mwanawe akamjibu "Mbona una niuliza swali hili hilo tuu ilhali nimekwisha kujibu kwamba NI NJIWA?" "hunielewi?"

Baadae Kidogo, mzee yule aliinuka na kwenda chumbani kwake alipo hifadi Diary yake ambayo aliihifadhi tangu mtoto wake huyo alipo zaliwa. Akafungua Ukurasa mmoja kisha akampatia mwanawe yule ili asome ukurasa ule.

Hichi ndicho kilicho kuwa kimeandikwa katika Ukurasa Ule....
"Leo mwanagu mwenye umri wa miaka mitatu alikuwa amekaa na mimi kwenye sofa, na alitokea njiwa katika Dirisha letu njiwa  huyo alikua akipia kelele. Mwanangu aliniuliza mara 23 "Baba ni nini Hicho?" nilimjibu mara zote 23 alizo niuliza, Nilimkumbatia kwa upendo kwa mara 23 zote alizokuwa akiniuliza jambo hilo hilo moja "Baba ni nini Hicho?". Sikumuonyesha kughadhabika kwa kuuliza swali hilo kwa mara 23 ilhali nlikwisha kumjibu."

Baada ya mtoto yule kumaliza kusoma ukurasa ule, alijawa na aibu ndipo akamwomba baba yake msamaha.


Tunajifunza nini katika hadithi hii?
Wazazi wako wanapo fikia katika uzee, hupaswi kuwaonea ama kuwadharau juu ya uzee wao. Huko unapo pitia tambua ya kwamba wao wailipitia pia enzi za utoto na ujana wao hivyo basi wewe unarudia rudia mambo(Huna jipya mbele ya macho yao). Haijalishi una elimu kubwa kiasi gani, ama una mali nyingi kuliko wazazi wako ila tambua ya kwamba Bila wao usingekuwa hivyo ulivyo. 

Tizama jinsi mzazi huyu alipo muuliza mwanawe swali moja kwa kurudia mara nne na mwanawe huyo akakasirika, ila mzee yule aliwahi kumjibu mwanawe swali hilo hilo kwa mara zote 23 ambazo mwanawe alimuuliza bila hata ya kuonyesha ghadhabu juu ya mwanawe, badala yake alimkumbatia kwa upendo na kumjibu.

“I will serve my old parents in the BEST way.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...