02 March, 2016

Tambua thamani ya kipaji chako leo.

Image result for TalentMnyonge mnyongeni, haki yake mpeni. Hakika Haja ya mja hunena na Uungwana ni vitendo. Uhali gani kijana mwenzangu? kwanza pole kwa majukumu ya hapa na pale ya kuhakikisha mkono unakwenda kinywani na hata njia ya chooni isiote nyasi. Leo tena kijana wenu nakaa tena jamvini ili niweze kunena la Moyoni hivyo embu na wewe kijana mwenzangu kaa chini tulizungumze hili swala!
Awali ya yote tambua kua Makala hii ni mwendelezo wa makala iliyopita ambayo ilisema Mambo yakufanya wewe kama kijana ili Kufanikiwa katika maisha.
     Nakumbuka wakati nikiwa mtoto niliwahi kuulizwa Mawere ukiwamkubwa unataka kuwa nani? kwangu mimi jibu lilikua nataka kua Mwana sheria. Kwanza kabla yakuendelea, tambua yakua kuna tofauti kubwa kati ya Ndoto na Kipaji, na mara nyinginge mambo haya huenda kwa wakati mmoja ila kwa asilimia chache kwa walio wengi. Wengi tumekua tukiamini kua ndoto ndio kipaji cha mtu ila jambo hili ni uongo mtupu yaani tunajidanganya, ndoto huja baada ya kipaji mfano kama wewe ni mchezaji mpira maarufu, kipaji chako ni kucheza mpira na ndoto yako siku moja ni kuchezea timu ya Taifa, au kama wewe ni mwanamuziki mchanga, kipaji chako ni Muziki na ndoto yako ni Kufanya Muziki kimataifa.
   Mpaka hapo umepata picha ya tofauti kati ya Kipaji na ndoto?
Embu ni kuulize swali , Je unatambua kipaji chako? na kama ni ndio una mpango gani na hicho kipaji cha kipekee ulicho nacho? Utanijibu kupitia anwani yangu ambayo nitakupatia baada ya kunena mawili matatu haya.
post-feature-image     Vijana wengi tumekua tukiishi tuu kama wadudu, unakutana na kijana mtaani kila muda kakalia mambo yasiyo mhusu, mara utamkuta akiongea siasa na huku hata hafahamu chochote kuhusu siasa. Naamini kila mwanadamu kaumbiwa kipaji chake lakini ni wachache wanaweza kutambua vipaji vyao na kuvifanyia kazi kikamilifu na hata leo tumeona matunda ya kazi zao. Mfano mzuri ni wanamichezo wa hapa nyumba kama vile Mbwana samata, Hashim Thabeeti, na wengine wengi wanaong'ara kupitia vipaji vyao. Embu kijana mwenzangu kaa chini na ujitatmini kwa kina na mapana kua wewe ni nan na unataka nini na ufanyeje ili kukikuza kipaji chako.
     Pengine matatizo yako yanayosibu leo ni wewe umeshindwa kutambua kipaji chako na kukiendeleza.. Tatizo hili limetukumba wengi mno, na hii inasababishwa na wazazi wetu, unakuta mzazi anamlazimisha mwanae kufanya kitu ambacho ni nje ya kipaji chake, unakuta mtoto ana kipaji cha kompyuta ama muziki lakini wazazi wanataka mtoto wao awe labda mwalimu au daktari. Kwa kweli hapa ndipo vipaji vya wengi hupotea na kama unavyojua tena mtoto mdogo hukua na kile alichopandikizwa akilini mwake tangu akiwa mdogo, Rai yangu kwa wazazi ni kwamba mtoto ajengwe katika misingi ya kipaji chake, mfano: kama mtoto anapenda muziki na anaonekana kweli ana kipaji cha muziki basi apelekwe katika shule zenye michepuko ya muziki na iwe hiyo kwa vipaji vingine.
       Kwa wale wenzangu na mimi ambao mnafahamu thamani ya vipaji vyenu basi msiishie hapo mlipo embu zidi kuchukua hatua nakusonga mbele na hakika ukijumlisha na bidii utakazo tia utafika ulipotamani kufika wakati ukiwa mdogo.
 NB; Kipaji huendana na ndoto, na bila ndoto hutosonga mbele, msomi mmoja aliwahi kusema " It is not a calamity to die with a dream, but it is a great disaster to die without a dream"  hivyo wenga malengo na ishi katika ndoto zako leo. Acha kupuyanga kila siku katika mabo yasio na msingi.

Kwa leo naomba nikomee hapo na panapo majaliwa week-end hii nitakuja tena hapa jamvini;
Kwa maoni na ushauri usisite kunitumia barua pepe ama ujumbe kupitia:-
 Email: mtokambali2015@gmail.com
 simu namba 0767322193

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...