Msanii Chid Benz amesema huwa hapendi kuisikiliza nyimbo yake ya Dar
es salaam Stand Up na kwamba hata anapo ‘perform’ jukwaani hujisikia
vibaya.
Chid Benz ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha Planet
Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, na kusema ukubwa wa wimbo huo
unamuumiza hisia zake, hivyo hujisikia vibaya kila anapousikiliza.
“Hii nyimbo sipendi kuisikiliza kwa sababu inaniumiza ni ngoma kubwa
flan kubwa sana, hata nikiwa na perform ile watu wanashangilia , kelele
nini ndiyo inanipa ushindi ila inanipa hisia tofauti”, alisema Chid
Benz.
Chid Benzi amesema ngoma hiyo aliiachia kwa baraka za mama yake,
baada ya kumuambia aitoe kwani ndiyo ilikuwa ngoma bora kati ya nyimbo
80 alizokuwa amerekodi kabla haijatoka.
“Dar es slaam stand up ilikuwa ndani ya nyimbo hizo 80 nilizorekodi,
siku moja mama yangu akaniambia ule wimbo unaoanza unalia tttt uko wapi?
nikamwambia, ngoja nikutafutie, akaniambia hii itoe, nzuri hii
nikaichukua nikaipeleka kwa Duly nikamkuta Pancho, nikamuita Ditto akaja
kuweka sauti na tukaifanyia kazi”, alisimulia Chid Benz.
05 March, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7
KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...
-
C9 Records presents STAR by Foby!. Click DOWNLOAD button bellow to download this song.
-
John ana mke ambaye haoni uzuri wa kitu chochote anachofanya, akifika tu nyumbani mke wake huanza kumlalamika kuwa hela anayoacha nyumba...
-
Mboga za majani na matunda zimekuwa zikisisitizwa kwa sana na wataalamu wa afya hasa kwa wanawake wajawaziti kwani zimekuwa zikiongeza Damu...
No comments:
Post a Comment