Serikali ya Zimbabwe yapinga marufuku ya WhatsApp

Serikali ya Zimbabwe imekataa pendekezo la kampuni za simu kupiga marufuku huduma ya Over The Top{OTT} kama vile WhatsApp na Skype ,waziri mmoja amenukuliwa katika gazeti la Herald akisema.
Kampuni hizo zilitoa ombi la huduma ya OTT zisimamiwe akihoji kwamba zinawazuia kupata faida.
''Tulisema kwamba sisi kama taifa endelevu ambalo linakuza teknolojia tunapuuza wazo hili la kuzipiga marufuku teknolojia hizi ,waziri wa habari na teknolojia Supa Mandiwanzira alisema.
Wabunge nchini Afrika Kusini pia wamekuwa wakilijadili ombi hilo la makampuni ya simu kusimamia huduma hizo za OTT ambazo zinaonekana kuwa rahisi kwa matumizi

Comments

Popular posts from this blog

Viashiria 6 ni kwa nini unatakiwa kubadili Maisha yako Leo

Furaha ya kweli inaletwa na wewe mwenyewe.