Edrisah Musuuza kwa jina Maarufu anajulikana kama Eddy Kenzo amezaliwa huko Masaka nchini Uganda. Mama yake alifariki kipindi ambacho Eddy alikua na miaka minne(4) tuu jambo ambalo lilimfanya msanii huyo kuanza kuishi mtaani na kuwa mtoto wa mtaana na hii ilitokana na Eddy kutokua anamfahamu baba yake wala ndugu yeyote kwa wakati huo na huko mtaani alikaa mpaka alipokuwa ana umri wa miaka 13.
Baada yakumaliza high school Eddy alijitwalia jina la kiusanii ambalo ni Eddy Kenzo na ndipo hapo akaanza kuandika muziki. Mnamo Mwaka 2008 alishirikishwa kwenye nyimbo ilijitwalia umaarufu nchin Uganda na Africa kwa ujumla wimbo uliokwenda kwa jina la "Yanimba" uliomilikiwa na msanii Mikie Wine.
Eddy Kenzo alizidi kujipatia umaarufu baada ya mwaka 2010 kuachia ngoma yake iliyokwenda kwa jina la "Stamina" ambapo wimbo huu aliutumia Rais wa Uganda Yoweri Museveni kipindi cha kampeni. Aliachilia Album yake ya kwanza mnamo mwaka 2012 iliyokwenda kwa jina la Ogenda Kunzisa na mwaka 2013 aliachilia album nyingine ilokwenda kwa jina la Kamunguluze na alifanikiwa kufanya toure nchini Marekani.
Wimbo wake wa "Sitya Loss" ndio wimbo uliozidi kumfanya Eddy awe maarufu Africa na Ulimwenguni kote na hasa pale alipowashirikisha gheto Kids wa Uganda kwenye video yake. Video hiyo ilipata kutazamwa kwa wingi na ilikua ikitazwa mara 10,000 kwa siku. Hivyo album yake ya tatu iliyokwenda kwa jina la "Sitya Loss" aliachilia mnamo mwaka 2014.
Eddy aliwahi kushirikishwa na kutambuliwa katika tuzo zifuatazo:
RAWMA International Reggae and World Music Awards 2014 Nominee
Channel O – Best East African Artist Nominee 2014
AFRIMMA Awards – Best Upcoming Artist Nominee 2014
Kunde Awards – Best East African Artist Winner 2014/2015
Zina Awards – Artist of the Year 2014/2015
Rising Star Awards – Song and Video of the Year 2014/2015
BET Awards – Best New International Act Viewers Choice
Kwa sasa anatamba na vibao vyake kama vile "SORAYE" na "ROYAL" ambapo katika wimbo huo wa "ROYAL" kamshirikisha msanii Patoranking.
Tazama nimbo yake ya "SORAYE" hapo chini Pia tizama video yake inayotamba kwa sasa inayokwenda kwa jina la "ROYAL" ambapo kamshirikisha msanii Patoranking.
No comments:
Post a Comment