
Ushindi huo ni sawa na kisasi cha kufungwa kwa penalti 3-1 katika fainali ya Kombe la Ligi, maarufu kama Capital One Cup Februari 28, Uwanja wa Wembley baada ya sare ya 1-1.
Katika mchezo wa leo, mabao ya Liverpool yamefungwa na Adam Lallana dakika ya 34, James Milner dakika ya 41 na Roberto Firmino dakika ya 57

Arsenal imefungwa 2-1 nyumbani na Swansea City Uwanja wa Emirates katika mchezo mwigine wa ligi hiyo. Mabao ya Swansea yamefungwa na Wayne Routledge dakika ya 32 na Ashley Williams dakika ya 74, wakati la Gunners limefungwa na Joel Campbell dakika ya 15.
Stoke City imeilaza 1-0 Newcastle United, bao pekee la Xherdan Shaqiri dakika y 80 Uwanja wa Britannia.
West Ham United imeilaza 1-0 Tottenham Hotspur, bao pekee la Michail Antonio dakika ya saba.
No comments:
Post a Comment