05 March, 2016

Arsenal watamkosa mlinda lango wao Petr Cech kwa wiki tatu hadi wiki nne kutokana na jeraha

CechArsenal watamkosa mlinda lango wao Petr Cech kwa wiki tatu hadi wiki nne kutokana na jeraha, meneja wa klabu hiyo Arsene Wenger amesema.
Kipa huyo wa umri wa miaka 33 atakosa mechi tatu za Ligi ya Premia, pamoja na mechi muhimu ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya ugenini dhidi ya Barcelona.
Aidha, atakosa mechi ya marudiano Kombe la FA dhidi ya Hull.
Aliumia mguuni alipokimbia kurejea kwenye ngome yake baada ya kuruka juu kudaka mpira wa kona wakati wa mechi ya Jumatano ambayo walichapwa 2-1 na Swansea nyumbani.
The Gunners wamo nambari tatu ligini, alama sita nyuma ya viongozi Leicester, na alama tatu nyuma ya Tottenham walio nambari mbili.
Arsenal, wanaojaribu kushinda taji la Ligi ya Premia mara ya kwanza tangu 2004, watakuwa ugenini dhidi ya Spurs Jumamosi.

Tarehe Wapinzani Michuano
Jumamosi, 5 Machi Tottenham (Ugenini) Ligi ya Premia
Jumanne, 8 Machi Hull (Ugenini) Marudiano (Kombe la FA)
Jumamosi, 12 Machi West Brom (Nyumbani) Ligi ya Premia
Jumatano, 16 Machi Barcelona (Ugenini) Champions League last 16
Jumamosi, 19 Machi Everton (Ugenini) Ligi ya Premia
Jumamosi, 2 Aprili Watford (Nyumbani) Ligi ya Premia

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...