Beki wa klabu ya Chelsea Kurt Zouma
atakua nje ya uwanja kwa miezi sita baada ya kuumia goti kwenye mchezo
dhidi ya Manchester United.
Zouma, atafanyiwa upasuaji kwenye
kwenye goti lake ambalo aliumia Jumapili uwanjani Stamford Bridge baada
ya kutua vibaya aliporuka kupiga mpira kwa kichwa.Uchunguzi umethibitisha kwamba aliumia vibaya na hivyo anapaswa kufanyiwa upasuaji kutibu tatizo hilo.Kawaida, Mchezaji akipata majeruhi ya aina hii, basi huwa nje ya uwanja si chini ya Miezi hivyo mchezaji huyu atakosa michezo yote ya msimu uliobaki.
Zouma, ambaye amekuwa kama pacha wa John Terry uwanjani, ameichezea Chelsea mechi 32 msimu huu.
Ameshaichezea Ufaransa mechi 2 za Kimataifa.
No comments:
Post a Comment