Mahali pekee utakapopata habari za Burudani,Michezo,Urembo udaku na Kuelimika
03 February, 2016
SIMBA YAKALIA NAFASI YA PILI NYUMA YA YANGA.
Simba imeendelea kuthibitisha inautaka ubingwa wa ligi ya Vodacom
msimu huu baada ya leo kufanikiwa kuchomoza na ushindi wa bao 5-1 dhidi
ya Mgambo JKT ikiwa ni ushindi wa nne mfululizo kwa Mayanja kwenye mechi
za ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara baada ya kujiunga na Simba kama
kocha msaidizi akitokea Coastal Union.
Mabao ya Simba yamefungwa na Hamisi Kiiza ambaye ametupia bao mbili
wavuni na sasa amemfikia Amis Tambwe wa Yanga kwa kufikisha bao 14 na
kinyang’anyiro cha mfungaji bora kuwa kitamu zaidi.
Magoli mengine ya mnyama yamekwamishwa kambani na Daniel Lyanga,
Ibrahim Ajib na Mwinyi Kazimoto ambao wote wamefunga bao moja moja.
Ibrahim Ajib katika harakati za kumtoka mchezaji wa Mgambo JKT wakati wa mchezo wao wa ligi kuu Tanzania bara
Ushindi huo unarejesha matumaini makubwa kwa Simba ya kunyakua
ubingwa kwasababu imefikisha pointi 39 sawa na Azam ambayo ipo nafasi ya
pili licha ya Simba kuwa mbele ya Azam kwa michezo miwili lakini patamu
ni pale Simba ambapo inatofautiana kwa pointi moja na watani wao wa
jadi Yanga ambao leo wamebanwa mbavu na kulazimisha sare dakika za lala
salama dhidi ya Tanzania Prisons.
Yanga bado inaongoza ligi kwa pointi 40 ikifuatiwa na Azam yenye
pointi 39 sawa na Simba ambayon ipo nafasi ya tatu lakini ikitofautiana
na Azam kwa magoli ya kufunga na kufungwa japo Simba wanaizidi Azam kwa
michezo miwili.
Matokeo ya mechi zote zilizochezwa leo yapo hapo chini:
No comments:
Post a Comment