08 February, 2016

Mandla Mandela aslimu na kuoa mke wa nne

Mjukuu wa kiongozi mwanzilishi wa Afrika Kusini Nelson Mandela , Mandla, 42, ameslimu na kuoa mke wa nne ambaye muislamu.
Mandla alifunga ndoa yake nne kwa bi Rabia Clarke katika msikiti mmoja mjini Cape Town Afrika Kusini mwishoni mwa juma.
Chifu huyo wa kabila la Mvezo ambaye pia ni mbunge alitoa taarifa akiishukuru familia ya Rabia kwa kumruhusu afunge ndoa na mwana wao.
''natoa shukrani kubwa kwa familia ya Rabia kwa kunikaribisha kwa dini ya kiislamu''
Video imeonekana katika mitandao ya kijamii inayomuonesha mrithi huyo wa kiti cha babu yake akiikariri ''Allah Akbar'' maanake ''Mungu ni mkubwa na hakuna aliye na uwezo zaidi yake''
Shekh Ibrahim Gabriel aliyeendesha nikaa hiyo katika msikiti wa Kensington siku ya Jumamosi alithibitisha kuwa Mandla alislimu mwaka uliopita na kuwa ndoa hiyo iliendeshwa kwa misingi ya sharia ya kiislamu.
Watumizi wengi wa mitandao ya kijamii walihoji iwapo tofauti yao wawili itaruhusu ndoa hiyo kusimama.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...