Manchester United walijikwaa katika
juhudi zao za kufana Ulaya baada ya kushindwa ugenini na klabu ndogo
kutoka Denmark katika Europa League.
United walichapwa mabao 2-1 na timu ndogo ya Midtjylland. Klabu hiyo ilianzishwa 1999.Klabu hiyo ya Old Trafford pia ilipata pigo baada ya kipa wake namba moja David de Gea kuumia kufundo cha mguu wakati akipasha mwili moto na nafasi yake kuchukuliwa na Kipa wa Argentina Sergio Romero.
Man Utd walitangulia kufunga kupitia Memphis Depay lakini Midtylland wakasawazisha kupitia Pione Sisto.
Paul Onuachu alifungabao la ushindi.
Manchester United walishindwa na Sunderland 2-1 Jumamosi Ligi ya Premia na wamepungukiwa na alama sita kufikia nambari nne, nafasi ya kufuzu Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Meneja wao Louis van Gaal majuzi alisema kushinda Europa League ndio njia rahisi kwao kufuzu kwa ligi hiyo ya mabingwa Ulaya msimu ujao.
United walikuwa bila nahodha wao Wayne Rooney ambaye anatarajiwa kutocheza kwa wiki sita kutokana na jeraha.
Kwenye mechi nyingine zilizochezwa Alhamisi usiku, Borrusia Dotmund wakicheza katika uwanja wao wa nyumbani, walipata ushindi wa 2-0 dhidi ya FC Porto
Matokeo mengine ni:
- Tottenham 1-1 Fiorentina
- Valencia 6-0 Rapid Vienna.
- Liverpool 0-0 Augsburg.
- Anderlecht 1 –0 Olympiakos
- Sevilla 3- 0 Molde
- St Etienne 3-2 Basel
- Villarreal 1- 0 Napoli
- FC Sion 1-2 Sporting Braga
- Galatasaray 1-1 Lazio
- Marseille 0-1 Ath Bilbao
No comments:
Post a Comment