06 February, 2016

Guardiola:Kazi ya Man City haitaniathiri


Mkufunzi wa timu ya Bayern Pep Guardiola amesema hatua yake ya kuelekea katika kilabu ya Manchester City haitaathiri kazi yake katika kilabu ya Bayern Munich msimu huu.
Guardiola mwenye umri wa miaka 45,amekubali mkataba wa miaka mitatu wa kuchukua mahala pake Manuel Pellegrini mwishoni mwa msimu huu.
Katika misimu misita ,kocha huyo wa zamani wa Barcelona ameshinda mataji 19 ikiwemo vikombe sita vya ligi na viwili vya bara Ulaya.
''Kwa nini vigumu?Mimi ni kama mwanamke,naweza kufanya kazi mbili mara moja na kudhibiti hali zote mbili.Nina talanta kubwa katika hili,''alisema Guardiola.
Guardiola ameripotiwa kukataa kandarasi mpya na kilabu hiyo ya Bundesliga mwaka uliopita na kutangaza mwezi Disemba kwamba ataondoka.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...