Mtandao
wa kijamii wa Facebook umeongeza huduma nyingine ambayo imepokelewa kwa
furaha na baadhi ya wateja. Facebook sasa inawawezesha baadhi ya wateja
wake kuwasiliana kupitia video za moja kwa moja, huduma ambayo
haikuwepo hapo awali isipokuwa tu kwa wakazi wa Marekani waliotumia simu
aina ya Iphone.
Lakini
sasa iwapo akaunti yako imedhibitishwa na Facebook, unaweza kuwasiliana
moja kwa moja na ndugu na marafiki kupitia mtandao huo.
facebook videos
PlaylistDownload
Wakati wa
uzinduzi wa huduma hiyo, wakurugenzi wa kampuni hiyo walisema wana
mpango wa kuisambaza katika maeneo yote ya ulimwengu kwa wote
wanaoutumia mtandao huo hive karibuni.
Mmoja wa walioipokea habari hizo kwa furaha ni Deral Eves ambaye ni mtaalam wa maswala ya kiteknolojia nchini Marekani.
Bw Eves
amesema: "Programu hii mpya inakuwezesha kuona matangazo ya video ya
moja kwa moja kutoka pembe zote za ulimwengu. Hii ni kumanisha kwa mfano
unaweza kutazama maonyesho ya muziki kutoka Russia au hata mtu
akitayarisha kahawa nchini Parauay."(VICTOR)
Na
ingawaje hili si jambo geni kwa baadhi ya watu wanaotumia mtandao,
itakuwa ni mara ywa kwanza kwa mamilioni ya watu kuweza kuwasiliana kwa
njia hiyo hususan kwa sababu ya wingi wa watu waliojisajili na mtandao
wa kijamii wa facebook.
Makampuni
kama vile Meerkat and Periscope yalianzisha huduma ya video ya moja kwa
moja mwaka jana. Yalifuatwa kwa karibu na mtandao wa kijamii wa
Twitter.
Mwezi
Agosti mwaka jana, kampuni hiyo ilizindua mpango wa kuwasiliana kwa
kutumia video, lakini huduma hiyo iliwafaidi tu wale waliokuwa wanatumia
simu aina ya Iphone na ni wale tu waliokuwa hapa Marekani ambao
wangeweza kufanya hivyo.
Huduma
hii mpya imekaribishwa na wengi, huku baadhi wakielezea matumaini yao
kwamba sasa wataweza kuwasiliamna na ndugu na marafiki wengi Zaidi ya
vile ilivyokuwa hapo awali.
No comments:
Post a Comment