
Wasanii hao walikutana nchini Kenya kwenye msimu huu wa Coke Studio, ambapo jumla ya wasanii 28 kutoka Uganda, Kenya, Tanzania, Msumbiji na Nigeria walikutana kwa ajili ya kufanya kazi pamoja za Coke.
Hapo ndipo uhusiano wa Yemi na Bien ulipoanza, lakini Yemi ameweka wazi baada ya msanii huyo kutokana nchini Kenya kumuandikia wimbo wake wa ‘No Gode’ kwa Kiswahili, ambapo Yemi aliuandika kwa Kiingereza.
“Nakupenda sana mpenzi wangu Bien, umetoa mchango mkubwa katika kazi yangu mpya kwa kuifanya iwe kwa Kiswahili na ulitumia muda wako kufanya hivyo, nitaendelea kukupenda daima,” aliandika Yemi kwenye mtandao wa Instagram.
No comments:
Post a Comment