Kutengeneza mafanikio katika maisha huchukua muda mrefu hivyo basi jitahidi sana kuangalia jinsi ambavyo unafanya mambo yako kuwa na imani kwamba ipo siku utaona nguvu zako zimekulipa.
Tambua kwamba watu waliofanikiwa hufanya maamuzi magumu, hivyo basi jitahidi kuwa na msimamo katika maisha fanya maamuzi katika kila sekta.
Jifunze kutokana na makosa pia tambua kwamba mafanikio huja baada ya kuona na kukabiliana na hayo makosa au changamoto.
Watu wanaokuwa na wewe katika mafanikio ni wengi sana ila tambua sana watu wanaokuwa na wewe katika matatizo au changamoto za maisha ni wachache na hao ndio wale marafiki zako wa kweli.
Ni vigumu kufanikiwa kwa kufanya vitu ambavyo hupendi hivyo basi siku zote fanya vitu ambavyo unavipenda kama kazi na mafanikio utayaona.
No comments:
Post a Comment