Ijumaa iliyopita kupitia kipindi cha WikiendChartShow cha Clouds Tv
kiliwakutanisha Nuh Mziwanda na Shishi ambao wameachana,Je? Kuna
uwezekano wapenzi hao wakarudiana?
’Nimeficha mambo yake mengi sana kwa maslahi ya penzi letu,yeye anajua
mambo gani aliyokuwa akinifanyia ambayo alikuwa hastahili kunifanyia
kama mpenzi wake,alikuwa akinichukulia poa tu,nilikuwa nikionekana
mwanaume mbele za watu lakini haikuwa kweli,nilikuwa naumia ndani kwa
ndani bila watu kujua,nimemsamehe sina tatizo nae,’’Nuh.
‘’Nuh na Shishi ni marafiki zangu nawajua vizuri walipokuwa wakigombana
nilikuwa niwasuruhisha yanaisha sasa kipindi hiki walivyogombana
sikuwepo nilikuwa Kigoma,ningekuwepo yasingefikia haya ila ninachojua
hawa wanapenda cha msingi mmoja wao ajishushe,’’Baba Levo.
‘’Unajua ukiongea na Nuh ukimuuliza unampenda Shilole hana jibu kamili
lakini ninavyoona wanapenda na watarudiana tu,ila Nuh anawahofia ndugu
zake ambao hawamtaki Shishi na mambo mabaya ambayo aliyokuwa
akimfanyia,’’ Soudy Brown.
No comments:
Post a Comment