13 January, 2016

Shirika linaloshughulikia watoto la Umoja wa Mataifa limesema zaidi ya nusu ya watoto Sudan kusini hawako shule.


Kwa mujibu wa UNICEF, idadi hiyo ni kubwa kuliko nchi yoyote ile duniani.
Shirika hilo limesema watoto wa kike na wakiume wapatao milioni 1.8 hawajapata elimu darasani.
Shirika hilo limesema toka kuzuka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2013 zaidi ya shule mia nane zimeteketea.
Serikali mjini Juba ilisaini mkataba na waasi mwezi Juni, lakini hata hivyo ghasia katika maeneo mengine ya nchi bado hazijakoma.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...