09 January, 2016

MAJIBU YA ZIZOU KUHUSU RONALDO KUONDOKA REAL MADRID

zinedine-zidane
Kocha mpya wa Real Madrid mfaransa Zinedine Zidane ‘Zizou’ amesema kuwa Cristiano Ronaldo katu hatoondoka Real Madrid hivi karibuni katika utawala wake na kumtaja mchezaji huyo kuwa ni ‘moyo’ wa timu.
Zinedine Zidane akiongea kuelekea katika mchezo wake wa kwanza kabisa akiwa meneja wa Madrid dhidi ya Deportivo La Coruna mchezo utakaochezwa Jumamosi January 9 amesema kuwa Cristiano hana bei yake na kwamba katu hatoondoka Real Madrid hivi punde.
Kocha wa Manchester United Louis Van Gaal mwezi November mwaka jana alidokeza uwezekano wa kumrudisha Cristiano Ronaldo Old Trafford lakini akasema tusubiri kuona nini kitatokea kutokana na ugumu wa kuwasajili wachezaji wakubwa kama Ronaldo.
Cristiano Ronaldo ambaye ni mshindi mara tatu wa tuzo ya mchezaji bora wa dunia ‘ballon d’Or’ ameshinda taji moja la La Liga pamoja na ubingwa wa Ulaya na ubingwa wa dunia ngazi ya vilabu akiwa na Real Madrid tangu asajiliwe mwaka 2009 akitokea Manchester United kwa ada ya uamisho wa pauni milioni 80.
Akiwa Madrid mreno huyo amevunja rekodi ya ufungaji wa mabao iliyokua inashikiriwa na Raul Gonzalez na kuwa mfungaji bora wa muda wote katika historia ya Galacticos.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...