Mahakama kuu ya Venezuela imeamuru
masuala yote ambayo yatatekelezwa na bunge la nchi hiyo ambalo
linadhibitiwa na upinzani hayatatambuliwa rasmi hadi pale wabunge watatu
wanaoshtumiwa kutochagua kihalali watakapoondolewa.
Uamuzi huo
bila shaka utaongeza sintofahamu iliyopo baina chama tawala cha Nicolas
Maduro,na kile cha muungano wa upinzani kilichoshinda viti vingi bungeni
katika uchaguzi wa December.Bunge jipya la nchi hiyo linadaiwa kupuuza amri ya mahakama kuu iliyotoa zuio kuapishwa wa upinzani,ambao walikuwa wakihofia kuikosatheluthi mbili ya kura zote za bunge.
No comments:
Post a Comment