Good news ni kwamba yale mabilioni ya elimu bure ya rais Magufuli tayari yameshawafikia watu wangu wa Mwanza….kazi inabaki kwako wewe mzazi kuhakikisha mwanao nae anayatumia kwa ufasaha ili ajikwamue baade, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo ndio mwenye uthibitisho kamili; – Mkuu wa mkoa Mwanza Magesa Mulongo
‘Kwa upande wa sekondari kwa mkoa wetu tuna jumla ya sekondari 197 kwa ujumla wake mkoa kupitia shule za sekondari kwenye akaunti zao za shule wamepokea milioni 642,648,000…ndani
ya fedha hizi kuna fedha ya ruzuku, fidia ya ada za kutwa na bweni
pamoja na chakula kwa shule za bweni kwa wilaya zetu zote na mkoa mzima,
nimatumizi ya mwezi January serikali itaendelea kutoa fedha kila mwezi
unaohusika;-RC Magesa Mulongo
‘Kwa upande wa shule za msingi tuna jumla ya shule 850 katika mkoa wetu, hizi nazo tarehe 30 December 2015… akaunti zote za shule za msingi kwenye wilaya na mkoa wetu wote ziliingiziwa kiasi cha shilingi milioni 356,728,000…Fedha ya chakula na ruzuku, kwa hiyo kwa ujumla wake hii ndio fedha ambayo tayari imeshatolewa kama ambavyo serikali iliahidi; – RC Magesa Mulongo
‘Maafisa
elimu na wakuu wa shule wanatakiwa kuhakikisha matumizi halali na
sahihi ya fedha hizi..Kila mwezi tutaendelea kufanya ufuatiliaji kabla
ya kuingiza fedha nyingine, mbele tutakuwa wakali sana kwa wazazi
watakaoshindwa kuwapeleka watoto wao shule; – Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mgesa Mulongo
No comments:
Post a Comment