16 January, 2016

Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania mzunguko wa kumi na nne unatarajiwa kuendelea wikiendi hii kwa michezo nane kuchezwa.


Katika uwanja wa Karume jijini Dar es salaam, Maafande wa JKT Ruvu watawakaribisha Maafande wa Mgambo Shooting,
Toto Africans watakua wenyeji wa Tanzania Prisosns uwanja wa CCM Kirumba, huku Stand United wakicheza dhidi ya Kagera Sugar uwanja wa Kamabarage mjini Shinyanga.
Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Simba SC watawakaribisha wakata miwa wa Mtibwa Sugar ,Mbeya City watakipiga na Mwadui FC uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Huko Tanga Coastal Union watawalika Majimaji mchezo utaopigwa katika dimba la Mkwakwani, huku Azam FC wao watapima ubavu na African Sports mchezo ukianza saa 1 usiku.
ligi hiyo itaendelea tena siku ya Jumapili kwa mchezo mmoja uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, ambapo Young African watawakaribisha Ndanda FC kutoka Mtwara.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...