13 January, 2016
KOCHA MPYA WA SIMBA APANIA KUIBADILI TEAM HIYO
Kocha msaidizi wa Simba Mganda Jackson Mayanja ameanza kwa kasi majukumu ya kukinoa kikosi hicho kwa kuwakimbiza wachezaji wake akitaja uwezo wa chini wa hali ya ufiti wa wachezaji wake ndiyo jambo atakaloanza nalo.
Akizungumza mara baada ya mazoezi ya leo asubuhi katika Uwanja wa Amaan Mayanja amesema, Simba aliyoikuta isingeweza kupata matokeo yaliyokuwa yakihitajika katika hali ya ufiti wa wachezaji aliyoikuta ambayo haiendani na ukubwa wa timu hiyo.
Kiungo huyo wa zamani wa KCC ya Uganda amesema hilo ni jukumu lake la kwanza aliloanza nalo lakini akawataka wanasimba kumpa muda na kuwa wavumilivu wakati huu akibadilisha baadhi ya mambo katika kikosi chao hicho.
Amesema amewataka wachezaji wake kuwa tayari kupokea mazoezi yake na kwa haraka ameridhika na viwango vya wachezaji akisema kila kitu kitaenda sawa kama watashikamana.
“Simba ina hadhi yake hii ni timu kubwa sasa hata kiwango chake kiwe ni kile kinachosubiriwa na mashabiki na viongozi wao, kuna mambo yalipungua hapa sitaki kuzungumza sana tutafanya marekebisho mengi mazoezini sio katika vyombo vya habari,” amesema Mayanja.
“Wito wangu kwa Wanasimba wasiikimbie timu yao sasa warudi tushikamane lakini pia wawe na subira kidogo wakati huu tunabadilisha mambo hapa haya yanahitaji muda kidogo hatuwezi kupata matokeo wakati vifua vya wachezaji vikiwa vyepesi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7
KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...
-
C9 Records presents STAR by Foby!. Click DOWNLOAD button bellow to download this song.
-
John ana mke ambaye haoni uzuri wa kitu chochote anachofanya, akifika tu nyumbani mke wake huanza kumlalamika kuwa hela anayoacha nyumba...
-
Mboga za majani na matunda zimekuwa zikisisitizwa kwa sana na wataalamu wa afya hasa kwa wanawake wajawaziti kwani zimekuwa zikiongeza Damu...
No comments:
Post a Comment