Leo Mbwana Samatta amemalizia simulizi yake ya siku tatu ya ‘Safari ya Samatta kutoka Mbagala kwenda Ulaya’. Leo ameeleza namna ambavyo timu ya Genk ilivyokuwa serious kumtaka akaitumikie ukilinganisha na timu nyingine za Ulaya ambazo zilikuwa zinamuhitaji.
Samatta pia ametaja sababu ambazo zimemfanya akubali kujiunga na timu hiyo na kuzikacha offer za timu nyingine ambazo zilikuwa zikimuwania.
Option zilikuwepo lakini timu nyingi walikuwa wanatumia zaidi mitandao yani walikuwa wananitafuta kupitia mitandao, lakini Genk wameonesha interest ya moja kwa moja, walisafirisha mtu kutoka Belgium hadi Dar es Salaam kuja kufatilia masuala yangu ya mkataba, mkataba wangu upoje ili wanapoanza process za kunisajili kusiwe na matatizo kwenye masuala yanaohusu mikataba.
Wakatoka Dar wakaja hadi Japan kuja kuonana na mimi mwenyewe moja kwa moja kipindi hicho tulikuwa kwenye mashindano ya klabu bingwa dunia. Wakaja kuniambia wameweka kitu hiki na kile kwa ajili yangu. Ni timu ambayo ilinifanya nijisikie kwamba kweli wananihitaji ukilinganisha na timu nyingine.
Halafu timu ambayo inakuhitaji moja kwa moja inakuwa inakuhitaji ili ikakupe nafasi tofauti na timu nyingine ambazo labda zinawachezaji wake lakini labda kuna mapungufu labda mchezaji ameumia au ametoka kwahiyo wanakuhitaji kwa ajili ya kuziba pengo tofauti na timu ambayo inakuhitaji moja kwa moja na lengo langu mimi ni kupata nafasi kwsababu bila kupata nafasi kwa asilimia zaidi ya 70 ni ngumu kuonesha kiwango changu na ni ngumu kupata opportunity nyingine.
No comments:
Post a Comment