Chama
Cha Mapinduzi (CCM) kimesikitishwa sana na ujumbe wenye maudhui ya
ubaguzi ulioandikwa kwenye moja ya Bango lililobebwa na mmoja wa
wananchi waliojitokeza katika maadhimisho ya Sherehe za Miaka 52 ya
Mapinduzi ya Zanzibar.
Chama
Cha Mapinduzi (CCM) kinaomba radhi kwa ujumbe huo, kinapinga na
kinakemea kabisa fikra, hisia na mitazamo yoyote yenye maudhui ya
kibaguzi.
Ujumbe
huo sio tu kuwa una maudhui ya kibaguzi bali pia unaenda kinyume kabisa
na falsafa na Shabaha ya waasisi wa Mapinduzi hayo Matukufu ya mwaka
1964 na unapingana na misingi na itikadi ya CCM inayohimiza Umoja na
Mshikamano wa Kitaifa.
Daniel Chongolo
Mkuu wa Mawasiliano na Umma CCM.
12/01/2016
Mkuu wa Mawasiliano na Umma CCM.
12/01/2016
CHANZO: MPEKUZI
No comments:
Post a Comment