Taarifa iliyopo sasa hivi ni kwamba Manchester United
wanakaribia kumsajili mchezaji kinda wa miaka 16 Luca Ercalani kutoka
club ya Forli inayocheza Serie D.
Mchezaji
huyu alionwa na scout David Williams na kupelekwa Manchester United kwa
ajili ya trial na inasemekana ameshafuzu na hivi sasa zinafanyika hatua
ya mwisho kukamilisha usajili wake.
Haitegemewi kufanyika tangazo rasmi la usajili wa mchezaji
huyu lakini kwenye page zake za instagram anaonekana kufurahia kwa
jinsi mambo yanavyoenda. Vyanzo vya karibu na habari hii vinasema kila
kitu kitakamilika ndani ya muda mfupi ujao.
No comments:
Post a Comment