13 December, 2015

Unawezaje kutambua kama anakupenda kwa dhati?

post-feature-imageHakuna njia ya uhakika zitakazo thibitisha kuwa mpenzi ambaye uponaye anakupenda kwa dhati kutoka moyoni na hakutanii. Kwakuwa mapenzi yanakuwa ya tofauti kwa kila mmoja na hata tafsiri ya mapenzi bado ni tofauti kwa kilammoja wetu hata mimi ninaye andika haya naweza nikawa nina danganywa na bado sijafahamu. Ila kwa poit hizi unaweza ukajua kama anakupenda kwa dhati au la!

Tambua tabia ya mpenzi wako.

Tambua kama anaweza kuwa yeye kweli akiwa na wewe.

Mapenzi ni kama maigizo, Kama mpenzi wako anauwezo wa kuwa mpole, mkarimu unapokuwa kwenye umati wa watu au hata akiwa na rafiki zake basi anakupenda. Hivi ndivyo tunavyosema uhalisia wake. Kama ukiwa naye tu wawili anaweza kukufokea basi anayo mapenzi ya dhati kwakuwa hakukuaibisha mbele za wengi. Kama anaweza kushiriki na wewe hisia zake za ndani basi anayo mapenzi ya dhati. Kama yupo wazi kuonekana kawaida yaani sio kuonekana yupo sahihi masaa yote, Kuonekana ana ganda la harage kwenye jino lake nk basi anakupenda kwa dhati.

Tambua kama yupo tayari kuwa na wewe karibu hata kwenye hali mbaya.

Kama mpenzi wako amekuwa anasiku mbaya na ameonyesha furaha pale alipo kuona, na sio kwakuwa anauhakika utamsaidia bali kwakuwa amekuona basi anayo mapenzi yakweli. Lakini kama anajitahidi kuongea na wewe kwakutaka kuona hakuna tatizo hatakama lipo basi inawezekana akawa hana mapenzi ya dhati.

Tambua kama anaweza kucheza na wewe hadharani. 

Mapenzi wakati mwingine nikama utoto, Hutojali upo wapi, Je mpenzi wako anaweza kucheza na kutaniana na wewe mkiwa popote! Kama anaweza kufanya hivyo basi huyo anakupenda. Kumbuka anafanya hivyo sio kwaajili ya mauzo bali kwaajili ya kuonyesha anakupenda. Kama anafanya hivyo kwaajili ya mauzo basi hakupendi.

Tambua kitu anacho kisema.

Angalia kama anapenda kuzungumzia juu ya ndoto za kuwa na wewe pamoja baadaye.

Kama mpenzi wako anakupenda, Basi wazo lakuwa na wewe maishani halitajificha. Kama unakaa naye asubuhi hadi jioni, mnatoka kula naye bata, na mishe zote yeye anazungumzia kuwa na gari zuri, nyumba nzuri lakini haja wahi kuzungumza kuwa na wewe kwenye maisha ya baadaye basi hana mapenzi juu yako na anakupotezea muda.
Kama mtu anaongelea juu ya ndoto zake na anakujumlisha wewe kwenye mawazo yake hayo basi hayo ni mausiano mazuri.

Angalia kama mpenzi wako anasema 'Nakupenda/I Love You' na anamaanisha.

Elewa kuwa kunatofauti kubwa kati ya 'Love ya!' na 'I love You.' Kama amekuwa akitamka neno hilo sahihi na kukutazama machoni bila ya kuonyesha dalili yakuhitaji kitu kingine  kwako zaidi ya kuwa na wewe, Basi anakupenda kwa dhati.

Angalia kama mpenzi wako anaongelea namna alivyo ku miss muda haupo.

Kama wewe na mpenzi wako mekuwa mbali na bado anapata muda wa kukupigia simu, kukutumia sms, kukutumia e mail nk basi kuna mapenzi. Lakini kama upombali naye kwa week na hata sms hujapata basi jua hapo hakuna mapenzi!

Angalia kama anakukosoa ukkosea.

Kwenye maisha sikuzote tunaishi kwa kuelekezana pale tunapokosea, Kam aupo kwenye mausiano na ukakosea lakini hajawahi hata sikumoja kukukosoa, Basi hakuna mapenzi hapo. Lazima kurekebishana ili kutengeneza future nzuri kati yenu makosa yasirudie.

Tambua matendo yake.

Je anakusikiliza kilakitu unachosema.

Kusikilizana ni jambo lamuhimu kwenye mahusiano, Kama sikuzote kwenye mahusiano ukawa na mtu ambaye hakusikilizi na wala hataki hata kujua unazungumza nini basi hakun amapenzi zaidi ya kupotezeana muda.
Sehemu ya kuwa kwenye mapenzi sio kwaajili ya kuwa mzungumzaji tu, Bali pia kuwa msikivu.

Angalia kama anafanya mambo mazuri kwako.

Kama mpenzi anakupenda basi atafanya mazuri kwako, Mfano kuja nyumbani kwako kukuoshea vyombo, kukupikia, kukusaidia usafi nk. Lakini ukiona mpenzi wako amekuja kwako na kila akija anataka kununua chakula au mtoke mkale nje basi sio mpenzi wa kuwa naye na hana mapenzi bali anapenda mteremko.

Je anajua muda wa kukuacha ufanya mambo yako.

Ukiwa na mpenzi pia ambaye kila saa anaku sms, ana kupigia, anataka kujua upo wapi na upo na nani, Tambua kuwa hana uaminifu kwako ndio maana anataka kuchunguza na hata ukimwambia unakazi unafanya haamini. Kama anakupenda hatataka kuwa na wewe masaa yote ila atakupa muda na wewe ufanye shughuli zako za msingi maisha yasonge. Usimlinde mpenzi wako bali mpende mpenzi wako.

Angalia kama anakuunga mkono.

Kama anakupenda, hata kuwa na wewe wakati wa raha na kujirusha tu, Bali atakuwa kila unapohitaji masaada wa kufikia malengo yako nakusonga mbele kwenye maisha bila kujali kam autamzidi kwa kipato, elimu nk baada ya hapo.



TENGENEZA KIPATO KUPITIA INTERNET KWA KUTEMBELEA >>>HAPA<<<

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...