18 August, 2015

Birdman kafikishwa tena Mahakamani, safari hii na producer wake…!

BIRDMAN
Producer wa Birdman, DVLP anamshitaki rapper huyo dhidi ya deni la dola 200,000 (sawa na Tzs. Million 400) kwa kazi za production ambazo boss huyo wa Cash Money Records hakumlipa.
DVLP
Producer DVLP
Producer DVLP ndiye aliyesimamia wimbo wa “develop” lakini Birdman hakuwahi kumlipa kwa kazi hiyo aliyoifanya na Lil Wayne pamoja na wasanii wengine… hata hivyo producer huyo anadai walishawahi kuzungumza na Birdman kwa message za kuchat kwenye simu lakini hakuwahi kutoa ahadi ya lini atamlipa pesa hizo.
Kazi ya kwanza ya DVLP ilikuwa na Lil Wayne mwaka 2005 kwenye ngoma ya “Fireman” ya rapper huyo na toka kipindi hiko amekuwa akifanya kazi mara kwa mara na star huyo wa Cash Money Records.
LIL
Lil Wayne
Licha ya kufanya kazi na Lil Wayne, DVLP ameshawahi pia kufanya kazi na rapper Rick Ross kutoka Maybach Music Group na Pitbull na alishawahi pia kutengeneza beat ya ngoma “Rap God” kwa ajili ya Eminem.
Producer DVLP ameamua apeleke mashitaka yake Mahakamani kwani ameona kama dalili za yeye kulipwa pesa zake ni ndogo ukizingatia mvutano uliopo sasa kati ya Birdman na Lil Wayne upo mbali na mwisho.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...