10 July, 2015

Hii ndio sababu ya Eddy Kenzo wa Uganda kupewa tuzo yake kwenye redcarpet ya BET Music Awards 2015.

 Eddy-kenzo

Msanii kutoka Uganda Eddy Kenzo ametoa sababu za kupokea tuzo yake kwenye redcarpet ya Bet badala ya kwenye jukwa la show ya BET Music Awards 2015.
Eddy Kenzo amesema “Waandaji wa tuzo za Bet walimfahamisha kuwa tuzo ya kila kipengele ilikuwa na mdhamini na kampuni iliyodhamini tuzo ya kipengele cha Viewers Choice ; Best International Artist haikulipiwa muda wa jukwaani na ndio sababu ya kukabidhiwa kwenye redcarpet”
Eddy amesema ukiacha kupewa tuzo kwenye redcarpet ,alithaminiwa vizuri na kulazwa kwenye hotel moja na mastaa kama Nicki Minaj, Drake na Tyga.


TOA MAONI YAKO

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...