
Pamoja na wasanii wa Tanzania kuonesha kusita kutoa album zao sokoni,
Ben Pol amesema mwaka ujao atatoa yake akiwa chini ya uongozi mpya wa
Panamusiq.Muimbaji huyo wa Sophia amesema kuanzia mwezi wa kwanza mipango hiyo inaweza kuanza rasmi.

“Mwezi kwanza tunaanza promotion ya album ambayo itatoka mwezi wa sita
au mwezi wa 12 mwakani kwahiyo hii ni project ya mwakani.”Hivi karibuni Ben Pol alisafiri kwenda nchini Ujerumani kwenda kufanya
video ya wimbo wa msanii wa Tanzania aishiye nchini humo
aliyemshirikisha, Emanuel Austin.
Kwa sasa msanii huyo yupo jijini Nairobi, Kenya alikoenda kurekodi kipindi cha Coke Studio Afrika.
No comments:
Post a Comment