Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara
inatarajiwa kuendelea mwishoni mwa wiki hii kwa michezo sita kuchezwa
katika viwanja mbalimbali nchini, huku michezo mitatu ikichezwa siku ya
jumamosi na michezo mingine mitatu ikichezwa siu ya jumapili.
Jumamosi katika Uwanja wa Sokoine
wapinzani wa jiji la Mbeya, Prisons FC watakua wenyeji wa wagonga
nyundo Mbeya City mchezo utaochezwa majira ya saa 10 kamili kwa saa za
Afrika mashariki na Kati.
Katika Uwanja wa Nangwanda
Sijaona wenyeji timu ya Ndanda SC watawakaribisha wakata miwa wa Kagera
Sugar, huku jijini Tanga Mgambo Shooting wakiwa wenyeji wa maafande wa
JKT Ruvu mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani.
Jumapili katika uwanja wa Taifa
jijini Dar es salaa, Simba SC watawakaribisha Azam FC, mchezo ambao
unatabiriwa kuwa na upinzani mkali kusaka nafasi ya pili ili mwakani
kuweza kuwakilisha Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho
barani Afrika.
Jijini Tanga wagosi wa kaya
Coastal Union watawakaribisha timu ya Stand United kutoka mjini
Shinyanga, mchezo utakaochezwa kwenye uwanja wa Mkwakwani, huku kwenye
Uwanja wa Manungu mjini Morogoro wenyeji Mtibwa Sugar wakiwakaribisha
maafande wa Ruvu Shooting.
No comments:
Post a Comment