Herrera akifunga goli lake
MANCHESTER United ikiwa uwanja
wa nyumbani wa Old Trafford imetoka sare ya 1-1 dhidi ya Arsenal katika
mechi ya ligi kuu England iliyomalizika usiku huu.
Ander Herrera katika dakika ya 30′ alipata pasi nzuri kutoka kwa Ashley Young na kuifungia Manchester United bao la kuongoza.
United wakiwa na matumaini ya
ushindi, dakika ya 82′ Tayler Blackett aliyetokea benchi alijifunga goli
katika harakati za kuokoa na kufanya mechi hiyo imalizike kwa sare hiyo
Kama ilivyo kawaida kwa mechi za karibuni, United waliongoza umiliki wa mpira kwa 58% dhidi ya 42% za Arsenal.
Mbali na hilo, United wamepiga
mashuti 6 dhidi ya 4 yaliyolenga lango, wakati ambayo hayakulenga lango,
mashetani wekundu wamepiga 6 dhidi ya 2 ya Gunners.
Hata hivyo kila timu imepiga kona 5 katika mechi hiyo iliyovuta hisia za mashabiki wengi.Matokeo haya yanaonesha wazi kuwa Man United watamaliza nne
bora, wakati Arsenal watamaliza nafasi ya pili na Man City nafasi ya
tatu.
No comments:
Post a Comment