BAADA
ya kufungwa mechi mbili kanda ya ziwa, mabao 2-1 na Kagera Sugar, 1-0
dhidi ya Stand United na sare ya 1-1 ya mwishoni mwa wiki iliyopita
dhidi ya
Azam fc , hatimaye wakata miwa wa Manungu, Turiani, Mkoani
Morogoro, Mtibwa Sugar wameibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Tanzania
Prisons katika mechi ya kiporo ya ligi kuu iliyomalizika jioni hii
uwanja wa Manungu Complex.
Kabla ya mechi hii Mtibwa Sugar walikuwa nafasi ya 11 katika msimamo wakijikusanyia pointi 24 baada ya mechi 21.
Leo
ilikuwa mechi ya 22 na kuvuna pointi tatu kumewasogeza mpaka nafasi ya 6
katika msimamo, pointi moja nyuma ya Mgambo wanaoshika nafasi ya tano
kwa pointi 28 baada ya kutoka suluhu dhidi ya Azam fc jioni CCM
Mkwakwani Tanga.
Hali
imezidi kuwa dhoofu kwa Prisons ambao baada ya kipigo cha leo
wanaendelea kuwa nafasi ya 13 kwa pointi zao 21 baada ya kucheza mechi
22.
No comments:
Post a Comment